March 29, 2015


Klabu ya Al-Sadd  ya Qatar imekanusha uzushi kwa kiungo Xavi harnandez amekamilisha uhamisho wa kujiunga nayo.


Uongozi wa klabu hiyo umesema taarifa zinazosambaa kwamba Xavi anajiunga na klabu hiyo na tayari ameingia mkataba ni uzushi mtupu.

Umeeleza kwamba alikuwa nchini Qatar kwa ajili ya kuangalia mazingira ya eneo hilo akiwa na familia yake.
Imeelezwa kwamba Xavi alilazimika kwenda Doha akiwa na familia yake kuangalia kama inaweza kuishi pale angalau kwa mwaka mmoja.

Lakini utata ulianza baada ya Meneja mkuu wa mklabu hiyo, Abdulla Al-Berik,kutupia mtandaoni picha ya Xavi na kusema ameishajiunga na klabu hiyo.

Huku kukiwa na picha, meneja huyo alianzika maneno haya: “Tumefanikiwa kumsajili Xavi na hii ndiyo picha yake akiwa na Mkurugenzi wetu Mtendaji, Muhammed Ghoulam".


Hata hivyo klabu hiyo imeendelea kusisitiza kwamba kweli iko katika majadiliano ikijaribu kumshawishi Xavi kujiunga nayo ili amalizie soka lake katika klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic