Kocha Sylvester Marsh amefariki dunia leo
asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Marsh alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa
kansa ya koo na hivi karibuni alisafirishwa kutoka Mwanza hadi jijini Dar es
Salaam.
Hata hivyo, hali ya Marsh aliyewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Kilimanjaro Stars pia alizinoa timu kadhaa za Ligi Kuu Bara iliendelea kuwa mbaya
kadiri siku zinavyosonga mbele.
Pamoja na hivyo suala la afya yake
liliendelea kuwa siri kubwa huku baadhi ya wadau wakisumbuka kutafuta wodi
aliyolazwa.
Aliwahi kuugua taabani na kukawa na taarifa
za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtelekeza. Lakini baadaye lilikanusha.
Mdau, Abdulfatah Saleh ambaye ni mmiliki wa
Hoteli ya Sapphire Court ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ndiye alijitolea
kumhudumia katika matibabu yake.
Ingawa alikuwa hapendi watu wajue, lakini
mdau huyo ndiye alifanya kila, juhudi kuhakikisha Marsh anapata matibabu bora
hadi alipopata nafuu na kurejea kwao Mwanza.








0 COMMENTS:
Post a Comment