MPIRA UMEKWISHAAAAA
Dk 90, Ngassa anaifungia Yanga bao la tano, mara nyingine baada ya kuiwahi krosi ya Sherman.
Dk 76, Hassan Dilunga anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul na anakwenda kucheza nafasi ya Telela na nafasi ya Abdul anarudi Telela.
Dk 74, Juma Abdul anaumia na kutolewa nje kwa ajili ya matibabu
MABADILIKO: Dk 69, Yanga wanamtoa Msuva na nafasi yake inachukuliwa na Mliberia Kpah Sherman.
Dk 65 Musona aliyefunga bao la Platinum, anawakosa Yanga na mpira unagonga mwamba na kuokolewa na Juma Abdul.
MABADILIKO: Dk 62, FC Platinum wanamtoa Wisdom Mutasa na kumuingiza super sub, Aaron Katege (Yanga inabidi wawe makini naye).
Dk 56, nusura Yanga wapate bao lakini Ngassa anajaribu kuuinua juu, kipa anamshitukia na kuukoa.
Dk 52, Yanga wanaonyesha hasira kwa kuongeza bao la nne kupitia kwa Mrisho Ngassa ambaye anamchambua kipa ikiwa ni baada ya zaidi ya basi nane kugongwa na yeye kuupachika wavuni.
Dk 46, Tambwe anaifungia Yanga bao la tatu, ikiwa ni dakika moja tu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili.
Kipindi cha pili kinaanza kwa kasi kubwa, Yanga wanaonekana kuja kwa haraka na FC Platinum wanazidiwa nguvu na kupoteza umakini.
KIPINDI CHA PILI:
Mechi imeanza kwa kasi kubwa, ila Yanga wanaonekana ndiyo wako fiti zaidi kwa kujipanga vema.
FC Platijum
wanajilinda zaidi na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na hasa kutokea
pembeni.
Lakini hiyo
haionyeshi kuwashitua Yanga ambao wanaendelea kucheza kwa kuonana vizuri huku
wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga kupitia kwa Haruna Niyonzima na Mrisho
Ngassa.
Dakika ta 17, kipa wa FC Platinum anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti kali la Niyonzima
Salum Telela
anaifungia Yanga bao katika dakika ya 26.
Mambo yanazidi kuwa matamu kwa Yanga zaidi ya Mcharo, Niyonzima anaifungia Yanga bao la pili katika dakika ya 40 baada ya kumchambua kipa na 'kuutupia' wavuni. Ilikuwa ni baada ya Tambwe kupiga shuti kali, kipa akatema, akataka kuwagi, akalambwa chenga na Mnyarwanda huyo akafunga.
FC Platnum si wabaya, wanaonyesha nao kuchangamka na dakika ya 45, Walter Musona anafanikiwa kuwafungia bao zuri la mkwaju wa adhabu unaomshinda Barthez.
WANAKWENDA MAPUMZIKO 2-1

0 COMMENTS:
Post a Comment