March 28, 2015


Bondia Mada Maugo amemaliza ubishi kwa kumtwanga Japhet Kaseba kwa KO.


Maugo amemchapa Kaseba katika raundi ya nane katika pambano lililomalizika muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar.

Pambano hilo lilikuwa la kumaliza ubishi kati yao na Maugo alitawala raundi mbili za mwanzo, kabla ya Kaseba kutawala raundi ya tatu na nne.

Kaseba alishindwa kuvumilia mapigo ya Maugo baada ya kuchapwa kwa konde kali la kushoto na kuanguka katika raundi ya nane.


Juhudi zake za kuinuka zilishindikana na kumpa ruhusa mwamuzi kumaliza pambano hilo.

Katika pambano jingine, Karama Nyilawila naye alimshinda Ibrahim Tambwe kwa KO katika raundi ya pili.

Na Ashraf naye akammaliza Ally Ramadhani kwa TKO katika raundi ya pili tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic