March 28, 2015


Mohammed Matumla amewapa raha Watanzania baada ya kumchapa kwa pointi Wang Xing Hua kutoka China.



Matumla ambaye alikuwa akinolewa na baba yake mzazi, Rashid Matumla 'Snake Man' alionyesha kiwango cha juu kabisa wakati akimshinda Mchina huyo.

Katika pambano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar na kumalizika hivi punde, haikuwa kazi lahisi kwa mtoto huyo wa Matumla kutokana na kiwango cha juu kilichoonyeshwa na raia huyo wa China.

Pambano hilo la raundi 10 lilikuwa la vutanikuvute kuanzia raundi ya kwanza.

Watanzania na Wachina waliokuwa ukumbini pale hawakutulia vitini kutokana na ushindani mkali wa mabondia hao.

HAta hivyo ilipofika raundi ya nane, baadhi ya Wachina waliokuwa katika ukumbi huo walianza kuondoka wakiamini ndugu yao asingeshinda pambano hilo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic