March 18, 2015

 

MGAMBO...
FULL TIME:
Simba wanaendelea kupambana lakini tayari hali inaonekana ni tete.
DAKIKA 8 ZA NYONGEZA
Simba wanaendelea kupambana lakini tayari hali inaonekana ni tete.

Dk 90, Maganga anabaki yeye na Manyika lakini anashindwa kufunga na kumpa mkononi.
Pamoja na kuwa wengi, Mgambo wanaonekana kupoteza muda zaidi.


Simba wanaonekana kushambuliwa zaidi kwa kuwa wako pungufu.

GOOOOOOOOO Dk 67 Fullyzully Maganga anafunga penalti na kuiandikia Mgambo bao la pili.


Dk 66 Anaingia Peter Manyika kuchukua nafasi ya Said Ndemla
 PENAAAAT Dk 63, Ivo Mapunda analambwa kadi nyekundu na Mgambo wanapata penalti baada ya yeye kumuangusha mshambuliaji wa Mgambo.

Dk 46, Simba wanamtoa Ajibu na nafasi yake inachukuliwa na Elius Maguri.

DAKIKA TATU ZA NYONGEZA;
GOOOOOOO Dk 45 Ally NAssor anaifungia Mgambo bao safi baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 huku Ivo Mapunda akiwa amezubaaa. Uzembe ulianzia kwa beki Kessy aliyekuwa amezubaa. Hilo ni Shambulizi la kwanz akali la Mgambo kwa kipindi chote cha kwanza.



Dk 35, Singano anamtoka beki anampa pasi nzuri Banda ambaye anapiga krosi nzuri inamkuta Okwi lakini kufunga.

Mgambo wanaonekana kukamia sana, mabeki na viungo wake wanacheza kibabe zaidi na mara kadhaa wachezaji wa Simba wanalalamika.
Dk 23, Okwi anakosa bao la wazi baada ya krosi nzuri ya Ajibu

Dk 13 Okwi anaumia, kocha anataka kumtoa lakini Okwi analazimisha kuendelea kucheza.
Mechi inaendelea na kila timu inashambulia ingwa Simba wanaonekana kuwabana sana Mgambo.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic