Mwili wa kocha Sylvester Marsh umewasili leo
jioni jijini Mwanza.
Mwili huo umewasili na kupokelewa na wadau
mbalimbali wa soka wa Mwanza wakiongozwa na Khalfan Ngassa na Rashid Abdallah.
VIJANA WAKIWA NA MAJONZI MAKUBWA WAKATI WAKIUSUBIRI MWILI WA MARSH NYUMBANI KWAKE MTAA WA USUMAU, MIRONGO. |
Wadau kadhaa walisafiri hadi nje ya jiji la
Mwanza kuupokea mwili wa Marsh ambao uliondoka jijini Dar es Salaam na Toyota
Coaster ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mwili wa Marsh utaagwa kesho katika viwanja
vya Mirongo ambako alianza kucheza soka akiwa mdogo na baadaye kuanzia kituo
cha kukuza watoto.
0 COMMENTS:
Post a Comment