March 19, 2015


Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri amesema kikosi hicho hakipaswi kuwekeza kwenye ubingwa wakati huu.


Phiri amesema Simba watajichanganya kuanza kuwaza kuwa wanagombea ubingwa wakati kikosi chao hakikuwa tayari kwa ubingwa.

"Wanaweza kuwa mabingwa au nafasi ya pili, lakini hawapaswi kugombea ubingwa sasa. Itawachanganya.

"Wanachotakiwa ni kugombea kufanya vizuri, kushinda na kupata pointi tatu katika kila mechi kama itawezekana.
"Lakini wakubali, hawana kikosi cha kushinda kila mechi. Maana yake wakubali na matokeo mengi na huenda baada ya msimu huu, kikosi kitaimarika zaidi," alisema Phiri.

Alisema bado ana imani na Simba kuwa na kikosi bora, lakini kinahitaji uzoefu zaidi ili kuwa bora zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic