March 18, 2015

LISTI YA SIMBA VS MGAMBO...

Watu wengi hawapendi kukosolewa lakini wanaweza kuwa wavivu wa utekelezaji.


Kuna mambo mengi yanahitajika kubadilishwa katika soka la Tanzania. Huenda mengine yanaweza kuwa ya kipuuzi kabisa na hautegemei kuona yanaendelea lakini hakuna anayeyafanyia kazi.
LISTI YA BARCELONA VS MAN CITY....

Kwanini hawajayafanyii kazi? Jibu hawajali, hawaupendi mpira na wanachoangalia wao ni kuingiza fedha kutoka katika mpira. Huu ni upuuzi.

Unapokuwa jijini Dar es Salaam, mechi za Ligi Kuu Bara zimekuwa zikiandaliwa kwa mpangilio mzuri sana.

Kitu kidogo nitakupa mfano, karatasi ya listi ya wachezaji. Utaona imepangiliwa vizuri kabisa tena kwa kuchapishwa.

Lakini mechi nyingi za mkoani, karatasi zinachukuliwa zile za daftari au listi inaandikwa hovyohovyo tu. Hauwezi ukasema hii ni hadhi ya Ligi Kuu Bara.

Karatasi ya listi za wachezaji ya Ligi Kuu Bara, mechi kati ya Simba dhidi ya Mgambo haina tofauti na mechi ya mchangani. Upuuzi.

Chama cha Soka Tanzania, kinapata mgawo katika mapato ya mechi hiyo. Kununua karatasi na kufanya mambo kwa mpangilio haiwezekani?

Hakuna kiongozi anayeona hilo si sahihi, hawana aibu na wanakubali vipi ifanyike?

Kama hao wanakubali, vipi uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nao unakubali hali hiyo? Unaona sawa kwa kuwa mambo yanakwenda?


TFF inapaswa kuwa kiongozi anayeangalia uhakika na hadhi ya inachokiongoza. Mabadiliko yafanyike. Ala!

1 COMMENTS:

  1. Du hili la line up kuandikwa kwenye karatasi kama ligi ya mbuzi ama mchangani ni aibu. TFF na Bodi ya Ligi wameonesho udhaifu mkubwa katika hili, binafsi nikiona mchanganuo wa mgao wa fedha za mapato uwanjani huwa nasikitika sana. Gharama za maandalizi ya mchezo mchanganuo wake ni upi?, naamini ni pamoja na shajara za kutunza kumbukumbu za mchezo. Sijui kama karatasi hizo kweli zinatoa sura halisi ya hadhi ya Ligi yetu yenye udhamini kutoka kwa makampuni na zaidi watazamaji wa mchezo wenyewe.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic