Yanga
imetoa onyo sasa kwamba haitaki utani baada ya kuichapa Coastal Union kwa mabao
8-0.
Katika
mchezo huo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, leo. Yanga ilionyesha
imepania ushindi baada ya kwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa mabao matatu.
Kipindi
cha pili kilikuwa na mabao mengine matano na Amissi Tambwe alifanikiwa kufunga
mabao manne, Simon Msuva, Salum Telela na Mliberia Kpaj Sherman akaona mwezi
kwa kucheka na nyavu
Yanga
imezidi kujichimbia kileleni baada ya kufikisha pointi 43.
Azam
FC yenye inabaki katika nafasi ya pili baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya
City kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.
Sare
hiyo imeifanya Azam FC kufikisha pointi 37 lakini ina mchezo mmoja pungufu kwa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment