Ruvu
Shooting imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa kuzingatia Kanuni ya
14(9) ya Ligi Kuu kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo (changing
room) katika mechi namba 149 dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga.
Pia
Ruvu Shooting imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutoingia vyumbani
wakati wa mapumziko kwenye mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia
Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu.
Naye Meneja
wa Polisi Morogoro, Manfred Luambano alitolewa kwenye benchi la Polisi Morogoro
kwa kosa la kutoa lugha za kashfa kwa mwamuzi msaidizi namba moja Martin
Mwalyanje. Suala lake linapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya hatua za kinidhamu.
Kipa wa
Ndanda SC, Wilbert Mweta amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000
(laki tano) kwa kumkanyanga na kutaka kumpiga mwamuzi Eric Onoka kwenye mechi
namba 155 dhidi ya Polisi Morogoro iliyochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 37(5) ya Ligi Kuu.
Kabla ya kufanya kitendo hicho alikuwa ameonyeshwa kadi nyekundu.
Meneja wa
Kagera Sugar, Mohamed Hussein anapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa
kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi na kutaka kumpiga mwamuzi msaidizi namba 2,
Said Mnonga kwenye mechi namba 158 dhidi ya Azam FC iliyochezwa Uwanja wa Azam
Compex jijini Dar es Salaam.
Naye Kipa
Andrew Ntala wa Kagera Sugar amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh.
500,000 (laki tano) kwa kuingia kwenye vyumba vya waamuzi na kuwatolea lugha ya
matusi mazito ya nguoni baada ya mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu
wa Kanuni ya 37(5)(c) ya Ligi Kuu.
Mwamuzi wa
mechi kati ya Azam FC na Kagera Sugar, Stephen Makuka na mwamuzi msaidizi namba
mbili Said Mnonga wameondolewa kwenye orodha za waamuzi wa Ligi Kuu na
kufungiwa miezi 12 kwa kushindwa kumudu mchezo kwa uzembe. Adhabu hiyo
imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu.
Pia Kamishna
wa mechi hiyo Bevin Kapufi amefungiwa mwaka mmoja kwa kutoa taarifa isiyo
sahihi. Adhabu hiyo imetolewa kwa uzingativu wa Kanuni ya 39(1) ya Ligi Kuu.
Naye Kamishna wa mechi namba 159 kati ya Mbeya City na Simba, Joseph Mapunda
amepewa onyo kutokana na ripoti yake kuwa na upungufu.
Mgambo
Shooting imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kuchelewa kufika kwenye
kikao cha kitaalamu cha maandalizi ya mechi (technical meeting) dhidi ya Ruvu
Shooting. Mechi hiyo namba 161 ilichezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, na
adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(2)(a) ya Ligi Kuu.
0 COMMENTS:
Post a Comment