Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za
pongezi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans, Yusuf Manji kufuatia timu
yake kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Katika salamu
zake za pongezi, Malinzi amesema kutwaa Ubingwa wa VPL ni jambo muhimu na sasa
wanapaswa kuanza maaandalizi kwa ajili ya michuano ya kimataifa barani Afrika
mwakani.
Klabu ya
Young Africans imetwaa Ubingwa wa Ligi Kuu nchini kwa mara ya 25 (ishirini na
tano) jana, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya timu ya Polisi
Morogoro katika uwanja wa Taifa huku ikiwa na michezo miwili mikononi kabla ya
ligi kumalizika.
Waziri wa
Habari, Vijana Utamuduni na Michezo, Dr. Fennela Mkangara anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za kukabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom
Mei 6, 2015 katika mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Young Africans.
Ukweli wamefanya vizuri sana Yanga,hata kwa upande wa nidhamu wamejitahidi sana.
ReplyDeleteHongera sana wanajangwani,na wengine waige.