April 13, 2015

Mshambuliaji nyota wa TP Mazembe, Mbwana Samatta ameshabuliwa kwa mawe na mashabiki wa timu ya Shark.



Mbwana raia wa Tanzania anayefanya vizuri nchini DR Congo, amesema ameshangazwa na mashabiki wale kuingia na mawe uwanjani.

"Wamenijeruhi, nilihisi kitu kimenipiga kichwani. Nilivyoshika hivi kuangalia mkononi, damu. Nikajua nimeumia.

"Nimepatiwa matibabu, ninaendelea vizuri kabisa. Lakini hawa jamaa walikuwa na mawe mengi kabisa pale uwanjani," alisema Mbwana alipozungumza moja kwa moja na SALEHJEMBE kutoka Lubumbashi, DR Congo.

"Unajua mechi ilikuwa si nzuri kwetu. Jamaa walituotea fasta na kutufunga mbili. Baada ya hapo tutakaanza kupambana lakini tulifanikiwa kupata bao moja. Mwisho ikawa 2-1.

"Mechi imeisha, fujo zikaanza, wakaanza kurusha mawe na mwisho ndiyo ikawa hivyo."

Mshambuliaji huyo Mtanzania ni tegemeo la safu ya ushambulizi ya TP Mazembe.

BLOGU YA SALEHJEMBE INAMPA POLE SAMATTA NA KUMTAKA AAMINI HIYO NI SEHEMU YA MAPAMBANO, AENDELEE KUPAMBANA.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic