MWANAMUZIKI AKON (WA KWANZA KUSHOTO), ATAKUWEPO. |
Dar es Salaam, 13 April 2015 Finali ya shindano la Airtel Trace Music
Stars Afrika lililoshirikisha washiriki kutoka nchi 13 barani Afrika chini ya
majaji mahiri akiwemo Akon, Devyne Stephens na Lynnsha mwisho mwa
wiki hii watashirikiana kumtanga rasmi mshindi wa Airtel Trace Afrika.
Airtel kupitia taarifa yake iliyotumwa na ofisa uhusiano wake Jane
Matinde imesema “Shughuli nzima ya kumtangaza mshindi itaonyeshwa kupitia
chanel ya Trace inayopatikana katika kituo cha DSTV #325 siku ya jumamosi
tarehe 18 April 2015
Shindano hilo kabambe la Airtel Trace music star lilihusisha
washiriki wengi walioshiriki kupitia kupiga simu na kurekodi mojakwa moja
ambapo jumla ya simu zaidi ya milioni mbili na laki tatu za washiriki
wote zilipigwa na kufanya namba ya washiriki wa shindano hili kubwa Afrika
kuweza kuzidi mashindano ya Ulaya na marekani kama vile ya voice na idols.
Washiriki 13 kutoka nchi za Afrika waliingia katika kinyanganyiro cha
kutafuta mshindi tarehe 28 machi 2015. Usikose kushuhudia shindano hilo
la kusisimua lenye vionjo vya kila aina, mbwembwe na bashasha tele.
Finali hizi za Airtel Trace Stars zitaonyeshwa siku ya Jumamosi ambapo
watazamaji na majaji watachagua na kutangaza mshindi ambaye atapata dili
la kurekodi , kupata mafunzo ya muziki kutoka kwa mwanamuziki nguli wa nchini
Marekani lenye thamani ya zaidi ya dola za kimarekani 500,000/=
Progam hii ya finali itarushwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18 April
kuanzia saa tatu Usiku na kurudia siku ya Jumapili tarehe 19 Aprili kuanzia saa
kumi jioni katika chaneli ya Trace urban. Kipindi kitadumu kwa muda wa
dakika tisini.
0 COMMENTS:
Post a Comment