Rais wa
Shrikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi ameunga mkono kauli
iliyotolewa jana na Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Kusini mwa Afrika
(Cosafa) kupinga ubaguziwa utu na vurugu zinazoendelea nchini Afrika kuelekea
kwa michuano ya Cosafa.
Katika
kuunga mkono kauli hiyo, Malinzi amemwandikia barua Rais wa Cosafa, Seketu Patel
na nakala yake kwenda kwa Dk Danny Jordan Rais wa Chama cha Mpira nchini
Afrika Kusini (SAFA) akielekeze masikitiko yake juu ya mauaji na vurugu
yanatokoea nchini humo.
Aidha
Malinzi ameeleze imani yake kuwa, kwa kushirkiana kwa pamoja nchi za Kusini mwa
Afrika zitaweza kuutumia mchezo wa mpira wa miguu kama kiunganishi cha vijana,
na kipaza sauti cha kuhamasisha utokomezaji wa ubaguzi wa uraia wa mtu.
Mapema
jana Rais wa Cosafa, Seketu Patel alisema nchini Afrika Kusini baadhi ya miji
kumekua na taarifa ubaguzi, vurugu na kutokea mashambulio zinazofanywa ili
kuwataka wageni waondoke nchini humo, ila wao kama Cosafa wamepanga kuitumia
michuano hiyo kama sehemu ya kurejesha amani na utulivu kwa wakazi huko.
Cosafa ni
michuano inayojumuisha watu kutoka katika mataifa mbalimbali, kuelekea kwenye
michuano hiyo sie tupo nyuma ya Safa kuhakikisha michuano hiyo inafanyika na
kurejesha amani na utulivu, kuwafanya watu wote kuungana na kuwa kitu kimoja
"alisema Patel"
Michuano
ya Cosafa inatarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu katika jimbo la
Kaskazini-Magharibi (North-West Province) ambapo hakujaathirika na mashambulio
hayo, na serikali ya Afrika Kusini imesema itahakikisha ulinzi na usalama
unaendelea kuwepo na kuimarika kwa hali ya juu.
Chama cha
Soka nchini Afrika Kusini (Safa) kimelaani vurugu hizo zinazoendelea nchini
humo na kusema wao kama wenyeji wamejiandaa kuhakikisha michuano hiyo
inafanyika kwa amani na usalama, hata wakati wa Kombe la Dunia nchini Afrika
Kusini (2010), palikua na tishio la hali ya usalama lakini michuano
iliweza kufanyika na kumalizika kwa usalama.
Aliyekua
Rais wa Chama cha Soka cha Nambia (NFA) John Muinjo, ambaye kwa sasa ni
mwenyekiti wa kamati ya waamuzi wa Cosafa na mjumbe wa muda mrefu amesema
anaamini michuano hiyo itarudisha umoja kwa watu wanaoishi nchini Afrika
Kusini.
Michuano
ya Cosafa inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17, 2015 katika jiji la
Rusternburg (North-West Province) nchini Afrika Kusini katika viwanja vya
Olympia Park na Moruleng ikishirikia nchi za Botswana, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius,
Mozambique, Namibia, Seychelles, South Africa, Swaziland, Zambia and
Zimbabwe.
Nchi za
Ghana na Tanzania zinashiriki michuano kama nchi waalikwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment