April 19, 2015

BEKI WA MBEYA CITY, JUMA NYOSSO  (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA JONAS MKUDE WA SIMBA.
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema hadi anasikia kuchanganyikiwa kutokana na kikosi chake kuwa na mwelekeo unaoeleweka.


Simba imekuwa ikienda kwa mwendo wa kufunga na kufungwa, hali inayoonyesha kumchanganya kocha huyo.

"Wakati mwingine nashindwa hata niseme nini. Angalau niache kidogo nitafakari," alisema baada ya kikosi chake kuchapwa mabao 2-0 na Mbeya City mjini Mbeya.

"Kikubwa pekee ninachoweza kusema, hatutakata tamaa. Lakini ninaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wachezaji na viongozi ili kuweka mambo safi," alisisitiza.

Awali, Simba ilitangaza kujipanga kushinda mechi zote tano zilizobaki ili kushika nafasi ya pili. Lakini mechi ya kwanza kati ya hizo tano, tayari imeota mbawa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic