April 16, 2015


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetuma salamu za rambirambi kwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Khamis Mcha kwa kufiwa na baba yake mzazi Mcha Khamis.



TFF inampa pole Khamis pamoja na familia yake, ndugu,jamaa, marafiki na klabu ya Azam FC na kusema iko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, marehem Mcha alifariki dunia juzi kisiwani Zanzibar.

Mwanaye ni kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Azam FC pamoja na Taifa Stars.

Pia Mcha ni kati ya wachezaji ambao wamekuwa wakitoa mchango wao katika kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Hereos.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic