April 18, 2015


Mtibwa Sugar ya Turiani Morogoro ilianza Ligi Kuu Bara kwa kishindo na kuongoza kwa wiki kadhaa kabla ya kupotea, lakini kocha wake, Mecky Maxime amesema wanaodhani kikosi chake kitashuka daraja imekula kwao.


Kikosi hicho kipo nafasi ya sita katika ligi kikiwa na pointi 27, Jumatano iliyopita kilizinduka na kuifunga Prisons bao 1-0 japokuwa kilikuwa kikisuasua katika mechi zake za hivi karibuni.

Maxime alisema: “Nimekuwa nikitolewa maneno ya kejeli na baadhi ya watu kuwa tutashuka daraja, nataka kuwaambia kwamba hatushuki daraja ng’o hata iweje.”

Alisema wachezaji wake wote wako fiti ambapo kila mmoja ana morali ya kupata ushindi kwenye michezo yote iliyobaki ili kuhakikisha hawashuki daraja kwa lengo la kuwaziba midomo wanaowabeza.

“Tunajua ligi ina ugumu wake lakini kwa sasa lengo tetu ni kuhakikisha tunashinda michezo yote iliyobaki ili tubaki katika ligi, hakuna anayependa kufungwa na yaliyotokea ni sehemu ya mchezo tu,” alisema Maxime nahodha wa zamani wa Taifa Stars.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic