BERLUSCONI AKIWA AMEBEBA KOMBE, JIRANI YAKE NI ANCELOTTI ALIYEIWEZESHA TIMU HIYO KUBEBA UBINGWA WA ULAYA PIA. |
Waziri
Mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi amemtaka kocha wa Real Madrid,Carlo Ancelotti kurejea AC Milan.
Berlusconi
ambaye ni mmiliki wa AC Milan amemtaka kocha huyo kurejea na kujiunga na klabu
hiyo kama kweli atatupiwa virago na vigogo hao wa Hispania.
Kumekuwa
na taarifa kuwa Ancelotti anatupiwa virago kutokana na timu hiyo kumaliza msimu
ikiwa mikono tupu.
Imeelezwa
kuwa Rafa Benitez aliyewahi kukipiga Madrid ndiye anapewa nafasi kubwa ya
kurejea na kuinoa klabu hiyo.
Gazeti
maarufu la michezo la Italia, La Gazzetta dello Sport limeeleza mmiliki huyo yuko tayari
Ancelotti atue AC Milan kuchukua nafasi ya Fillippo Inzaghi.
0 COMMENTS:
Post a Comment