Uongozi wa Simba umesema uko tayari kukaa meza moja na
watani wao Yanga ili kulijadili suala la malipo ya haki za runinga kutoka Azam
Media Group.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na Mjumbe wa
Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe amesema wako tayari
kukutana na kila timu inayoshiriki Ligi Kuu ikiwemo Yanga.
“Hili suala halikuwa sahihi, tunahitaji kukaa na
kulijadili. Hata wakiwa Yanga sawa, pia timu nyingine zinazoshiriki ligi.
“Itakuwa vizuri sana kama tutakutana wote yaani timu
zinazoshiriki ligi, pia TFF na hao wadhamini.
“Kwangu naamini Simba na Yanga zilistahili kupata
zaidi ya fedha hizi zilizotolewa,” alisema Hans Poppe.
Alipoulizwa kuhusiana na Simba kuwahi kusaini mkataba
huo bila ya kufanya uchunguzi, alisema haya.
“Alikwenda kusaini harakaharaka alikuwa Rage, alikuwa
na kawaida ya kutokaa na kamati yake ya utendaji na kujadili.
“Amekwenda amesaini na sasa hili ni tatizo. Sisi
tungependa kulimaliza hili kwa uzuri kabisa,” alisema Hans Poppe.
0 COMMENTS:
Post a Comment