May 1, 2015

WACHEZAJI WA YANGA WAKIJIFUA LEO KWENYE UWANJA WA OLIMPIKI MJINI SOUSSE, TUNISIA

Yanga imefanya mazoezi yake ya mwisho leo Ijumaa kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Soussse, Tunisia kujiandaa na mechi dhidi ya Etoile du Sahel.


Mechi hiyo ya pili ya Kombe la Shirikisho inapigwa kesho saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.


Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi hayo chini ya Kocha Hans van der Pluijm na wachezaji walionekana kuwa fiti.

Hayo yalikuwa maandalizi ya mwisho ya Yanga kabla ya mechi hiyo na zaidi yalikuwa ni mazoezi mepesi.

Mechi ya kwanza jijini Dar es Salaam, iliisha kwa sare ya bao 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic