May 2, 2015

Inawezekana haukuwa kumsikia gwiji wa Real Madrid Raul Gonzalez Branco akimzungumzia Lionel Messi.


Raul amemuelezea Messi kama mchezaji tofauti na wa aina yake.
Amesema licha ya kuwa aliwahi kucheza na wachezaji nyota kama Zidane, Ronaldo, Figo, Ronaldo na wengine, lakini Messi ni mchezaji wa kipekee.
“Messi ni mchezaji tofauti kabisa. Anafanya kila kitu kionekane ni lahisi uwanjani.

“Ukimuona anavyocheza, unaweza kudhani yuko mtaani na wenzake anacheza tu kwa kukfurahisha.

“Wakati ule ndiyo nakua, watu waliofanya mambo kama hayo angalau Roberto Baggio au Ryan Giggs, lakini sasa Messi ni wa aina yake.

“Nina imani Madrid itafanya vizuri hata kuchukua tena kombe la Ulaya, ila Messi anaendelea kubaki kuwa mchezaji wa aina yake,” alisema Raul.


Messi naye aliwahi kumsifia Raul kuwa ni mchezaji mwenye upendo na wanamichezo na aliwahi kumpongeza kwa kuifunga Madrid.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic