Beki wa kati wa Simba raia wa Uganda, Joseph
owino, ameifungia mlango timu yake hiyo kwa kusema kuwa hana mpango wa kubaki
tena katika kikosi hicho msimu ujao.
Owino anatarajia kumaliza mkataba wake
mwishoni mwa msimu huu ambao alisaini msimu uliyopita. Hata hivyo, kuna wakati
alilazimika kurejea nyumbani kwao kwa madai ya kuuguza goti na aliporudi nchini
alikuta namba yake imeshachukuliwa na Juuku Murshidi na Hassan Isihaka ambao wametengeneza
pacha ya kuelewana katika beki ya kati.
Owino amesema kuwa, kuna timu anafanyanayo
mazungumzo kwa sasa na kudai kuwa ataiweka wazi mara baada ya kumalizika kwa
ligi.
“Sitarajii kuongeza mkataba mwingine katika
timu ya Simba, mimi naondoka na wala sihitaji kubakia tena msimu ujao, nilikuwa
najua nini kinaendelea na tangu ilipobakia miezi sita, nilikuwa najua
nitakwenda wapi baada ya hapa.
“Mkataba wangu unatarajia kuisha mwishoni mwa
msimu huu, hivyo nitaiweka wazi timu nitakayokwenda katika mechi ya mwisho
dhidi ya JKT Ruvu,” alisema Owino.
0 COMMENTS:
Post a Comment