Kiungo mshambuliaji wa Yanga mwenye kasi,
Simon Msuva anatarajia kuanza majaribio ya kucheza soka katika klabu ya Orlando
Pirates ya Afrika Kusini.
Msuva ameondoka leo alfajiri lakini
uongozi wa Yanga ulimsisitiziza kusubiri.
Orlando tayari walipeleka barua ya maombi
Yanga, lakini wakaonekana hawakutaka aondoke kabla ya ligi kwisha.
“Anatarajia kuanza majaribio kesho baada
ya kuwa amefika leo na kupumzika,” kilieleza chanzo.
Msuva amekuwa ana kasi na tegemeo katika
safu ya ushambuliaji ya Yanga.
Kwa sasa ndiye anayeongoza kwa ufungaji
bora na Orlando Pirates imekuwa ikitaka kujiimarisha katika ufungaji.
Blogu hii ilikuwa ya kwanza kuandika kuhusiana na Wasauz kumfuata Msuva jijini Dar es Salaam kuangalia baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara alizokuwa akicheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment