Wakati Klabu
ya Simba ikilia na kipato kiduchu milangoni, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limetangaza kushikilia mapato yao ya vyanzo vingine kuhakikisha zinapatikana
shilingi milioni 22 za madai ya wachezaji wake wa zamani, Amissi Tambwe na
Haruna Chanongo.
Chanongo
anaidai Simba milioni 11.4 zilizotokana na kutolipwa mshahara wake akiwa kwa
mkopo Stand United huku Tambwe anayekipiga Yanga kwa sasa anaidai dola 7,000
(milioni 11) kwa kusitishiwa mkataba.
Wiki
iliyopita, TFF iliiagiza Simba kuhakikisha wachezaji hao wanalipwa kufikia
Aprili 30, mwaka huu, vinginevyo watakatwa kwenye mapato ya mlangoni ili kupata
kiasi hicho.
Ofisa Habari
wa TFF, Baraka Kizuguto, amesema iwapo makato ya getini hayatatosha kufikisha
kitita hicho, watalazimika kushikilia mapato ya vyanzo vingine ili kuhakikisha
kabla ya ligi kufungwa wawe wamepata haki yao.
“Tayari
tumeanza kukusanya malipo yao, Simba ilikatwa kwenye mapato ya mlangoni kwenye
mchezo uliopita na Azam. Waligawana pasu kwa pasu, zilikatwa milioni tatu na timu
ikachukua tatu,” alisema Kizuguto.
Hivi karibuni
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alikaririwa
akisema kuwa timu hiyo kwa sasa imeyumba kiuchumi kutokana na mapato ya
mlangoni kushuka kwa kiasi kikubwa kutokana na uchache wa watu viwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment