Kundi maarufu la vichekesho nchini la Olijino Komedi sasa
limeamua kuingia kwa nguvu katika biashara ya kilimo.
Wasanii hao wamekabidhiwa Matrekta saba aina
ya Sonalika DI 50 RX na Kampuni ya Quality Extended Enterprise ya jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kilimo.
Baada ya kuyanunua, Orijino Komedi walikabidhiwa
Mtrekta hayo yenye thamani ya Sh milioni 170
katika hafla iliyofanyika makao makuu ya Quality Extended Enterprise yaliyopo
barabara ya Nyerere jijini Dar.
Kiongozi wa Orijino Komedi, Sekioni David
‘Seki’ alisema kuwa hatua hiyo ni moja
ya malengo yao ya kimaendelo waliyokuwa wamejiwekea hapo hawali wakati walipokuwa wakianzisha
kundi hilo.
Alisema malengo yao yalikuwa ni kuhakikisha
wanafikiwa zaidi kimaisha lakini pia wanakuwa mfano wa kuigwa kwa vijana
wengine hapa nchini.
“Tulianzisha kundi hili siyo kwa ajili ya
buradani pekee lakini pia kwa ajili ya maendeleo yetu binafsi hivyo baada ya
kupata matrekta haya tutajikita rasimi katika kilimo.
“Tayari tumesha mashamba mkoani Mbeya na
Iringa lakini pia tupo katika mazungumzo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mzee Yusuf Makamba ili aweze kutupatia shamba jingine huko kwao mkoani
Tanga ili tuweze kutimiza ndoto zetu,” alisema Siki.
Kundi
la Olijino Komedi linaundwa na wasaanii saba ambao ni Seki, Mpoki, Joti,
Masanja, Wakuvanga, Macklegan pamoja na Vengu.
0 COMMENTS:
Post a Comment