MALINZI |
Rais wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa
Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CC) timu Young Africans
katika mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya Etoile du Sahel utakaochezwa
kesho nchini Tunisia.
Katika salamu zake
Malinzi amesema ,Young Africans wakiwa ndio timu wawakilishi pekee wa Tanzania
na Afrika Mashariki katika michuano ya kimataifa barani Afrika wanapaswa
kupambana kuhakikisha wanasonga mbele katia hatua inayofuata.
Katika mchezo wa awali
uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, Young Africans ilitoka
sare ya bao 1- 1 na Etoile du Sahel, na mshindi wa jumla kwa mchezo wa huo,
atacheza hatua ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu zitakazokuwa zimetolewa
kwenye Ligi ya Mabingwa (CL) kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment