Utamu wa Ligi Kuu ya Bara unatarajiwa kuendelea wikiendi hii lakini kivutio kikubwa kikiwa ni mjini Mbeya.
Jumamosi katika Uwanja
wa Sokoine wapinzani wa jiji la Mbeya, Prisons FC watakua wenyeji wa wagonga
nyundo Mbeya City mchezo utaochezwa majira ya saa 10 kamili kwa saa za Afrika
mashariki na Kati.
Katika Uwanja wa
Nangwanda Sijaona wenyeji timu ya Ndanda SC watawakaribisha wakata miwa wa
Kagera Sugar, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa maafande wa
JKT Ruvu mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Jumapili katika uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaa, Simba SC watawakaribisha Azam FC, mchezo ambao
unatabiriwa kuwa na upinzani mkali kusaka nafasi ya pili ili mwakani kuweza
kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Jijini Tanga wagosi wa
kaya Coastal Union watawakaribisha timu ya Stand United kutoka mjini Shinyanga,
mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, huku kwenye Uwanja wa Manungu
mjini Morogoro wenyeji Mtibwa Sugar wakiwakaribisha maafande wa Ruvu Shooting.
0 COMMENTS:
Post a Comment