May 6, 2015


Utamu wa Ligi Kuu Bara kwa mabingwa kupigiwa makofi wakitoka vyumbani umefanyika leo.


Wachezaji wa Azam FC waliokuwa mabingwa watetetzi wamewapigia makofi wachezaji na memba wa benchi la ufundi la Yanga ambao ni mabingwa wapya.

Tukio hilo lilitokea wakati Yanga wakiingia uwanjani katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.


Utaratibu huo umekuwa ukitumika zaidi kwenye Ligi Kuu England na safari hii umetumika Tanzania Bara kwa bingwa kupigiwa makofi kama anakuwa amebaki mchezo au michezo baada ya kuwa ameishabeba ubingwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic