Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, leo Jumatano
kinatarajia kuingia kambini jijini hapa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake
wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya ya Misri.
Kikosi hicho kinaingia kambini leo huku kukiwa na uteuzi mpya wa
wachezaji ambao wameongezwa kwa ajili ya kuongeza nguvu.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto,
alisema kuwa kikosi hicho kimeteuliwa na kocha Mart Nooij kuongeza nguvu katika
kikosi cha timu hiyo ambacho kilikwenda nchini Afrika Kusini.
“Kocha Nooij ameamua kuteua kikosi cha wachezaji 16 ambao
wataingia kambini Jumatano (leo) kwa ajili ya kuanza kujiwinda dhidi ya Misri.
“Kikosi hicho kimeitwa ili kukiongezea nguvu kile kilichoshiriki
michuano ya Cosafa Afrika Kusini ambapo wachezaji wake wapo mapumzikoni, sasa
baada ya hapo wachezaji wote wataungana Juni Mosi na kutengeneza timu ambayo
itajiwinda kucheza michuano hiyo ya Afcon na Chan,” alisema Kizuguto.
Wachezaji ambao wameitwa katika kikosi hicho ni Jonas
Mkude, Peter
Manyika, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka (Simba), Salum Telela,
Juma Abdul, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Aishi Manula, Mudathir Yahya,
Frank Domayo na Kelvin Friday (Azam).
Wengine ni Rashid Mandawa, Atupele Green (Kagera
Sugar), Haruna Chanongo (Stand United), Malimi Busungu (Mgambo JKT) na Emmanuel
Simwanda (African Lyon).
0 COMMENTS:
Post a Comment