Timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars' itacheza mchezo wake wa kwanza wa kombe la Cosafa siku ya
jumatatu dhidi ya Swaziland katika uwanja wa Royal Bafokeng pembeni kidogo ya
jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.
Awali michezo ya kundi B
ilikuwa ifanyike katika uwanja wa Olympia Park, lakini waandaji wa michuano ya
COSAFA Castle wamesema kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wao michezo
hiyo imeshindikana kufanyika katika uwanja huo.
Uwanja wa Royal Bafokeng ni
miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali za Kombe la Dunia 2010 chini
Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji 42,000 huku timu ya
Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.
Leo asubuhi Taifa Stars
imefanya mazoezi katika uwanja wa shule ya Rustenburg chini ya kocha mkuu Mart
Nooij, na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo huo wa
jumatatu.
Kesho jioni Taifa Stars ifanya
mazoezi saa jioni katika uwanja wa Rolay Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja
kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya Swaziland.
Akiongelea hali ya hewa, kocha
mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea kuizoea hali ya
hewa, japokuwa kuna baridi hakuna mchezaji aliyeshindwa kufanya mazoezi
kutokana na hali ya hewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment