May 4, 2015


Aliyewahi kuwa mlezi wa Simba, Rahma Al Kharoos, maarufu kama Malkia wa Nyuki, amekutana na masaibu baada ya akaunti yake ya email ‘kutekwa’ na kuanza kutumika vibaya.


Akaunti yake ‘ilitekwa’ na wahalifu wa mtandaoni raia wa Nigeria na ikaanza kutumiwa kuwaomba fedha watu mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani.

Wahalifu hao walikuwa wakiwaomba fedha watu kadhaa waliowasiliana nao kwa madai wao ndiyo Malkia wa Nyuki, wako safarini barani Ulaya wamekwama kifedha.

Akizungumza kutoka Muscat, Oman, Malkia wa Nyuki alikiri kutokea kwa jambo hilo lakini akasisitiza ni wahalifu raia wa Nigeria ndiyo waliokuwa wakifanya hivyo.

“Hakika sikuwa mimi, hao watu waliichukua akaunti yangu. Kwa kweli sijui wanaingiaje na mwisho wakaanza kuwasiliana na watu kadhaa.

“Walikuwa wakifanya hivyo lakini uzuri watu wengi waliweza kuwasiliana na mimi na kunieleza nikalifanyia kazi,” alisema.

Wizi wa kimtandao umekuwa ukikua kila kukicha huku raia wa Nigeria ndiyo wakionekana kuwa namba moja katika utapeli huo.

Hata hivyo, Malkia wa Nyuki alisisitiza kwamba hakukuwa na madhara makubwa na alikuwa katika harakati ya kuikomboa anuani yake hiyo ya email.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic