May 2, 2015


Wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa, Yanga wametolewa baada ya kufungwa kwa bao 1-0 dhidi ya Etoile du Sahel.


Mechi hiyo ya pili ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Olimpiki mjini Sousse, Tunisia, imeifanya Yanga ing’oke kwa jumla ya mabao 2-1 ikiwa ni baada ya sare ya bao 1-1 jijini Dar.

Yanga ilionyesha mchezo mzuri lakini bao la kipindi cha kwanza lililofungwa na nahodha Amar Jemal kwa kichwa, ndiyo lililowang’oa.

Kipindi cha pili, bado Yanga ilionyesha soka safi lakini ilipoteza nafasi kadhaa.


Mshambuliaji wake, Amissi Tambwe alionekana kuwa msumbufu kwa mabeki wa Etoile. Lakini mwisho mechi hiyo imeisha kwa wawakilishi hao wa Tanzania kung’olewa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic