June 22, 2015


Baada ya kibarua chake kuota nyasi, Kocha Mart Nooij kesho atapata nafasi ya kuwaaga Watanzania.

Nooij atawaaga Watanzania katika mkutano na waandishi wa habari.
Taarifa kutoka TFF zimeeleza kwamba ingawa mkutano wa kesho ulikuwa kati ya Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi na waandishi wa habari lakini amemshawishi Nooij kuungana naye.

“President ndiye amemueleza Nooij aungane naye kwa ajili ya kuwaaga waandishi angalau.

“Amemkumbusha kwamba walikutana na waandishi siku ya kwanza na alizungumza na Watanzania kupitia waandishi. Hivyo ni vizuri awaage,” kilieleza chanzo.

Kibarua cha Nooij kimeota nyasi baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uganda katika michuano ya kuwania kucheza Chan.


Kabla ya hapo, Stars ilikuwa imechapwa mabao 3-0 na Misri katika michuano ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika maarufu kama Chan.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic