June 20, 2015


Wachezaji Taifa Stars wanaingia uwanjani mjini Zanzibar hivi punde tu kucheza dhidi ya Uganda 'The Cranes' wakiwa na morali baada ya ahadi ya mkwanja.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi ametoa ahadi ya Sh milioni 1 kwa kila mchezaji kama Stars itashinda.

“Kweli rais ametoa ahadi hiyo kwa wachezaji, wote wameipokea vizuri na tunatarajia kuwa watapambana kweli,” kilieleza chanzo.

Stars inaivaa Uganda katika mechi ya kuwania kucheza michuano ya Chan, mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Kwa Kocha Mart Nooij utakuwa ni mtihani wake wa kwanza kwa maana ya kile kilichoelezwa na TFF kwamba akitolewa, basi safari imemkuta.


Stars itacheza mechi hiyo ya nyumbani ambayo inatakiwa lazima ishinde ili kujiwekea mazingira mazuri kabla ya mechi ya marudiano mjini Kampala.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic