Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
limepitisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni watakaosajiliwa.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine
amesema wamepitisha hilo baada ya kamati ya utendaji ya shirikisho hilo
iliyokaa leo mjini Zanzibar.
“Wachezaji wasizidi saba, lakini pia wote
saba wanaruhusiwa kucheza kama timu itaamua kuwatumia,” alisema.
Kabla ya hapo timu moja ilikuwa inaruhusiwa
wachezaji wasiozidi watano baada ya TFF kupunguza kutoka kumi.
0 COMMENTS:
Post a Comment