Mshambuliaji mpya wa Simba, Laudit Mavugo ni shabiki
wa kutupwa wa Borussia Dortmund.
Mavugo amekuwa akivaa jezi ya Dortmund, moja ya timu vigogo
ambayo msimu uliopita haukuwa wa neema kwake.
Mshambuliaji huyo ambaye taarifa za uhakika zinaeleza
ameishasaini mkataba wa miaka miwili na Simba, ameonekana katika picha kadhaa
akiwa amepiga uzi huo wa njano na nyeusi unaotumiwa na Dortmund.
Atakapotua nchini, inaonekana wazi atakuwa na wakati
mgumu kuvaa uzi wa timu hiyo kwa kuwa Msimbazi, mambo ni nyekundu na nyeupe na
anayevaa jezi ya njano, anaonekana kama msaliti.
0 COMMENTS:
Post a Comment