Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ambayo inadhaminiwa na kampuni ya bia ya
Kilimanjaro, leo inaingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyopo eneo la
Gerezani kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri kuwania kufuzu kwa Fainali za
Mataifa Afrika (AFCON).
Kikosi
kitakachoingia kambini kinawajumuisha wachezaji waliocheza michuano ya Cosafa
nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Mei, wachezaji 20 walioanza kambi tangu
wiki iliyopita na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Congo DR.
Taifa
Stars inatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Gymkana na Uwanja wa Taifa
kwa muda siku mbili kabla ya siku ya alhamis kusafiiri kuelekea Addis Ababa
nchini Ethiopia ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya
Misri.
Wachezaji
wanaotarajiwa kuingia kambini leo ni Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomari
Kapombe, Oscar Joshua, Haji Mwinyi, Aggrey Morris, Salum Mbonde, Erasto Nyoni,
Saimon Msuva, Hassan Dilunga, Joram Mgeveke, Juma Liuzio, Said Ndemla, Mwinyi
Kazimoto, Abdi Banda, John Bocco, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Ibrahim Hajibu,
Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta.
Wachezaji
waliopo kambini tangu wiki iliyopita ni Nadir Haroub, Juma Abdul, Salum Telela,
Peter Manyika jr, Jonas Mkude, Hassan Isihaka, Mohamed Hussein, Aishi Manula,
Frank Domayo, Mudathir Yahya, Kelvin Friday, Malimi Busungu, Bennedict Tinoco,
Rashid Mandawa, Atupele Green, Haroun Chanongo, Emmanuel Simwanda, Said
Mohamed, Andrew Vicent, Gadiel Michael, Deus Kaseke.
Msafara
wa Taifa Stars unatarajiwa kuondoka nchini Alhamis Juni 4, 2015 kuelekea
Ethiopia ukiwa na wachezaji 23,benchi la ufundi pamoja na viongozi .
Mechi
kati ya Misri dhidi ya Tanzania inatarajiwa kuchezwa Juni 14, 2015 katika
uwanja wa Borg El Arab pembeni kidogo ya jiji la Alexandria.
Wakati
huo huo Tanzania imepata mwaliko wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa
ya Rwanda kati ya Juni 6, 7 mwaka huu jijini Kigali, kwenye kumbukumbu ya
mauaji ya kimbali, Tanzania itapeleka kikosi cha vijana U23 katika mchezo huo
utakaochezwa mwishoni mwa wiki.
Kufuatia
kupata mwaliko huo kikosi cha U23 kitaondoka nchini ijumaa tarehe 5, Juni 2015
kuelekea nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 18 chini ya kocha Salum Mayanga.
Kocha
wa Mtibwa Sugar Mecky Maxime ameongezwa kwenye benchi la ufundi litakalokwenda
Ethiopia kisha nchini Misri kufuatia kocha Salum Mayanga kuwa na timu ya
U23 nchini Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment