Baraza la Vyama Vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki
na Kati (CECAFA) kesho Alhamis tarehe 16 Julai, 2015 litaendesha mtihani wa
utimamu wa mwili (Pysical test) kwa waamuzi wa watakochezesha michuano ya kombe
la Kagame inayoanza mwishoni mwa wiki huu.
Zoezi hilo la utimamu kwa waamuzi watakochezesha mashindano
ya Kagame, litafanyika kuanzia saa 2 asubuhi katika uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam litasimamiwa na kamati ya waamuzi yay a CECAFA.
Waamuzi wanaotarajiwa kuhudhuria zoezi hilo ni Ali
Ahmed, Suleiman Bashir (Somalia), Ahmed Djama (Djibout), Yetayew Belachew
(Ethiopia), Kakunze Herve (Burundi), Davis Omweno, Peter Sabata (Kenya), Issa
Kagabo, Hakizimana Louis (Rwanda), Ahemd El Faith (Sudan), Lee Okelo na Mashood
Ssali (Uganda), Israel Mjuni na Ferdinand Chacha (Tanzania).








0 COMMENTS:
Post a Comment