July 8, 2015

CHUJI
 
Kiungo mkongwe wa Mwadui FC, Athuman Iddi ‘Chuji’ amesema amekuwa akifanya mazoezi kwa juhudi zaidi ili kuhakikisha anarejea Ligi Kuu Bara akiwa na kiwango cha juu.
Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Mwadui mkoani Shinyanga, Chuji amesema anajua ushindani mkubwa ulio ligi kuu.


“Ligi kuu ni tofauti la ligi daraja la kwanza. Hivyo lazima kujiandaa vizuri zaidi. Nimekuwa nikifanya mazoezi na wenzangu kama kawaida.
“Lakini nikipata nafasi nafanya mazoezi ya ziada kwa kuwa najua narudi kwenye kazikazi,” alijigamba.
Chuji aliachwa na Yanga, baadaye akajiunga na Mwadui FC inayonolewa na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.

Akiwa nahodha, amepambana na kuiwezesha Mwadui FC kupanda hadi Ligi Kuu Bara.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic