Mshambuliaji nyota wa
Yanga, Donald Ngoma ameonyesha kuwa kweli ni wamo baada ya kuanza dakika 90 za
kwanza akiwa na Yanga kwa kufunga bao.
Ngoma amefunga bao
pekee wakati Yanga ikiishinda KMIKM katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Ngoma alifunga bao hilo
akiunganisha kona iliyochongwa na Mbrazil, Coutinho.
Mshambuliaji huyo
amejiunga na Yanga akitokea Platnum ya Zimbabwe na alifanikiwa kuonyesha
kiwango kizuri lakini KMKM nao waliipa Yanga wakati mgumu.
0 COMMENTS:
Post a Comment