Michuano ya Kombe la Kagame
inayoendelea kutimua vumbi katika viwanja viwili vya Taifa na Karume vilivyopo
jijini Dar es salaam, itaendelea kesho kwa michezo miwili itayopigwa katika
dimba la Uwanja wa Taifa.
Katika michezo iliyochezwa jana,
Malakia ya Sudani Kusini iliibuka na ushindi wa mabao 2- 1 dhidi ya Adama City
ya Ethiopia, LLB ya Burundi ikitoka sare ya bila kufungana na Heegan FC
ya Somalia mchezo uliochezwa saa uwanja wa Karume, huku Azam FC wakiibuka na
ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya KCCA ya Uganda.
Vinara wa kundi A timu ya Gor
Mahia kutoka nchini Kenya, leo Jumatatu watashuka dimbani kucheza na timu ya
KMKM kutoka Visiwani Zanzibar ambayo pia juzi iliibuka na ushindi katika mchezo
wake wa awali dhidi ya Telecom.
Gor Mahia ambayo ilipata ushindi
wa mabao 2- 1 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga, itakutana na KMKM ambayo
iliibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya timu ya Telecom ya Djibout, mchezo
utakaochezwa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Mchezo wa kwanza utazikutanisha
timu za Telecom ya Djibout dhidi ya Khartoum-3 kutoka nchini Sudan, ambayo
itakua ikicheza mchezo wake wa kwanza.
Jumanne kutakua na michezo mitatu
ambapo Al Shandy watacheza na LLB katika kundi B saa 8 mchana uwanja wa Taifa,
Heegan FC dhidi ya APR uwanja wa Karume saa 10 jioni, Malakia dhidi ya Azam
kundi C Uwanja wa Taifa saa 10 jioni.
Jumatano mabingwa mara tano wa
michuano ya Cecafa Kagame Cup, timu ya Yanga SC watacheza dhidi ya Telecom ya
Djibout saa 10 jioni uwanja wa Taifa, KCCA wakicheza na Adama City saa 10 jioni
uwanja wa Karume, na Khartoum wakicheza mchezo wa awali saa 8 mchana uwanja wa
Taifa dhidi ya KMKM.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA
WA MIGUU TANZANIA (TFF)








0 COMMENTS:
Post a Comment