![]() |
| MKURUGENZI WA BODI YA LIGI, BONIFACE WAMBURA. |
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) itaanza Sept 12
badala ya Agosti 22 ili kumpa Charles Mkwasa fursa ya kuendelea na program yake
kuelekea mechi ya Taifa Stars vs Nigeria itakayochezwa Sept 5.
Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield)
itakayozikutanisha Azam FC dhidi ya Yanga SC sasa itachezwa Agosti 22 badala ya
Agosti 15.
Ratiba ya Ligi Kuu iliyokuwa imeandaliwa, sasa
inafanyiwa marekebisho kwa ajili ya tarehe mpya ya kuanza, ambapo pamoja na
mambo mengine mechi sasa zitachezwa wikiendi na katikati ya wiki na wikiendi ya
Oct 25 hakutakuwa na mechi kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Klabu za Ligi Kuu zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe
mpya ya kuanza Ligi, na dirisha la usajili linabaki kama lilivyo.
Wamiliki wa viwanja vyenye upungufu wmeandikiwa barua
kutakiwa kurekebisha upungufu katika muda maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa
kutumika kwa ajili ya PL na FDL.
Timu ya Madini ya Arusha imeruhusiwa kutumia Uwanja wa
Nyerere uliopo Mbulu mkoani Manyara kwa mechi za SDL kwa masharti upungufu
uliopo kwenye uwanja huo urekebishwe kwanza.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
(TFF)








0 COMMENTS:
Post a Comment