Michuano ya
Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Kagame Cup) inatarajiwa
kuanza kutimua vumbi siku ya Jumamosi tarehe 18 Julai 2015 jijini Dar es
salaam, kwa kushirikisha timu 13 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya
Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na kati.
Mashindano ya
CECAFA Kagame Cup ni mashindano makongwe barani Afrika ambayo yalianza mwaka
1967 kwa kushirikisha timu za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na mwaka huu
ni mashindano ya 40 tangu kuanza kwa michuano hiyo
Klabu ya
Simba ndio timu inayoongzoa kwa kutwaa ubingwa huo mara sita (6) ikifuatiwa na
Yanga, Gor Mahia zilizotwa mara (5), APR ya Rwanda ikiwa imetwaa ubingwa huo
mara tatu (3). Yanga na Gor Mahia zina nafasi ya kufikia Simba SC endapo
zitafanikiwa kutwaa Ubingwa msimu huu.
Mechi ya ufunguzi
ufunguzi siku ya jumamosi uwanja wa Taifa itawaktanisha APR ya Rwanda dhidi ya
Al Shandy ya Sudan saa 8 kamili mchana, KMKM kutoka Visiwani Zanzibar watacheza
dhidi ya Telecom ya Djibout uwanja wa Karume saa 10 jioni, huku wenyeji
timu ya Yanga wakiwakaribisha Gor Mahia kutoka Kenya saa 10 jioni.
Kuelekea
kwenye mashindano hayo, waandaji wa michuano hiyo CECAFA kwa kushirikiana na
wenyeji Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya
michezo hiyo, ambapo Uwanja wa Karume kiingilio kitakua shilingi elfu mbili
(2,000) na uwanja wa Taifa kiingilio cha chini kitakua ni shilingi elfu tano
(5,000) na kiingilio cha juu ni elfu 20,000 (20,000).
Timu
zinazoshiriki michuano hiyo;-
Kundi A:
Yanga (Tanzania Bara), Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar),
Khartoum-N (Sudan).
Kundi B:
APR
(Rwanda), Al-Shandy (Sudan),LLB AFC (Burundi), Heegan FC (Somalia).
Kundi C:
Azam
FC (Tanzania), Malakia (Sudan Kusini), Adama City (Ethiopia) na KCCA (Uganda).
Michuano hiyo
ya CECAFA Kagame Cup itaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha
Supersport.
0 COMMENTS:
Post a Comment