Mtanzania Charles
Misheto amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu ya Rabestein FC ya
nchini Ujerumani.
Rabestein FC
inashiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ujerumani na Mishetto aliyekuwa kiungo wa
zamani wa Stand United ya Shinyanga, tayari amesaini makataba huo.
Akizungumza
kutoka Ujerumani, Mishetto amefanikiwa kusaini mkataba na timu hiyo.
“Ingawa awali
nilikuwa nafanya majaribio na timu nyingine, lakini sasa nimefanikiwa
kusajiliwa na timu nyingine ya daraja la nne ambayo ilianza kuniwania,”
alisema.
“Nilikuja hapa,
nikafanya nao mazoezi kwa siku mbili, baada ya hapo wamekubaliana na uwezo
wangu, tumesaini mkataba.”








0 COMMENTS:
Post a Comment