July 20, 2015

Yule komediani mtukutu wa Uingereza, leo ametoa mpya baada ya kuvamia mkutano wa waandishi wa habari aliokuwa akiendesha Rais wa Fifa, Sepp Bllater aliyetangaza kujiuzulu na kumwaga noti feki za dola.

Simon Brodkin ambaye vipindi vyake vimekuwa vikimhusisha mwanasoka Jason Bent na Lee Nelson, alivamia mkutano huo, wengi wakiamini ni mmoja wa waandishi na kuanza kumwaga dola hizo za bandia.

Aliendelea kumwaga fedha hizo kwa Blatter kama sehemu ya rushwa huku akisema: “Hizi ni kwa ajili ya Korea 2026.”

Alikuwa akimaanisha anamhonga Blatter ili aipe Korea uenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 206.

Hali hiyo ilimfanya Blatter abaki amepigwa butwaa kabla ya walinzi kuingia na kumtoa Brodkin.

Kawaida Brodkin amekuwa akifanya hivyo sehemu mbalimbali. Hivi karibuni alimvamia jukwaani Kanye West wakati akitumbuiza na yeye kuanza kutumbuiza.

Kabla ya hapo, aliwahi kutoa kali alipoungana na wachezaji wa timu ya taifa ya England akizuga naye ni mchezaji lakini akashitukiwa hatua ya mwisho wakati akikaribia kupanda ndege.











ALIPOMVAMIA KANYE JUKWAANI...


ALIPOZUGA NI MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND...



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic