Bosi mkuu wa Bayern Munich, Karl-Heinz
Rummenigge amethibitisha kiungo wake mkongwe Bastian Schweinsteiger atajiunga
na Manchester United.
Schweinsteiger ameonyesha na nia ya kupenda
changamoto mpya zaidi ya Bundesliga.
Rummenigge amesema juhudi zilifanyika kumbakiza Schweinsteiger
lakini mwenyewe amesisitiza anataka kuondoka.
Schweinsteiger ameitumikia Bayern kwa miaka 13
mfululizo na sasa kiungo huyo mwenye miaka 30, anaona ni wakati mwafaka kuivaa
changamoto mpya.
Tayari imeelezwa atajiunga na Manchester kwa dau
la pauni milioni 15 na kuungana kwa mara nyingine na kocha wake wa zamani Louis
van Gaal.
0 COMMENTS:
Post a Comment