August 20, 2015


Uongozi wa Azam FC umesema hauna tatizo na uamuzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumbadilisha mwamuzi wa mchezaji wa Ngao ya Jamii, Jumamosi.


Mchezaji huo unawakutanisha Azam FC dhidi ya Yanga ambao utarushwa moja kwa moja na runinga ya Azam TV, sasa utachezeshwa na Martin Saanya.

TFF imembadilisha Israel Nkongo ambaye ameelezwa kuwa na matatizo ya misuli.

Katibu wa Azam FC, Idrissa Nassor amesema wao wanachotaka ni uchezeshaji wa kufuata sheria 17 za soka.

“Kwa kweli hatuna tatizo, kama sheria 17 za soka zitafuatwa sisi hatuna tatizo.

“Hiyo si kazi yetu, kikubwa ni maandalizi ambayo tumekuwa tukiendelea kuyafanya,” alisema Nassor.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic