August 19, 2015


Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf manji amerudishwa katika nafasi yake ya kuwania udiwani katika kata ya Mbagala Kuu.


Manji alishinda kwa kishindo, lakini akaenguliwa katika hali iliyoelezwa kuwa ya figisufigisu.

Hata hivyo, KAmati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyokaa jana, imemrejesha Manji baada ya wahusika kukimbia wakati wa kuhojiwa.

“Ulipofika wakati wa wahusika kuhojiwa, hawakuwepo, walipopigiwa simu walikuwa wamechelewa na kusema wanakuja lakini baada ya muda walizima simu.

“Hali hiyo ilifanya kamati kuu moja kwa moja kuchukua uamuzi wa kumrejesha Manji katika nafasi yake aliyoshinda kwa kishindo,” kilieleza chanzo.


Wananchi wa Mbagala Kuu walionyesha hasira zao kwa kuvamia makao makuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam wakitaka Manji arudishwe baada ya kugundua aliondolewa kwa fitita licha ya ushindi wake wa kishindo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic