August 19, 2015


Mkuu wa kitengo cha habari cha Yanga, Jerry Muro amewakaribisha watani wao Simba akiwataka wajitokeze kwa wingi katika mechi ya Ngao ya Jamii kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi.

Mechi hiyo inawakutanisha Yanga dhidi ya Azam FC na Muro amesisitiza kwamba ni mechi ya “Wa kimataifa”.
“Ni mechi nzuri na itakuwa ngumu, tuna uhakika wa kushinda. Kikubwa pia tunawakaribisha ndugu zetu Simba, acha nao waje.

“Waje waone wakimataifa wakipambana, wasijisikie vibaya kuja kuona. Hawana nafasi ya kuona mechi nzuri kama hiyo hata kama wao si wakimataifa,” alijinadi Muro.

Utani wa Simba na Yanga ulianza tokea mwaka 1936 baada ya kuanzishwa rasmi kwa Simaba ikitokea kwenye ubavu wa Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic